Posts

Showing posts from November, 2022

MIKOA MITATU YASIMAMISHWA UCHAGUZI CCM

Image
  Pichani : Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndug.Daniel Chongolo  akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dodoma. CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimefikia uamuzi wa kusimamisha uchaguzi katika mikoa mitatu kwa nafasi zilizoonyesha kuwa na changamoto pamoja na kufuta uchaguzi wa Umoja wa Vijana kwa kile kilichopelekea Kuonekana Kwa Viashiria vya Rushwa. Ndugu Chongolo amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa mara baada ya tukijiridhisha kama hakutakuwa na  changamoto ,chama kitaruhusu  uchaguzi kufanyika na kama watabaini  changamoto wataondosha wagombea wenye changamoto na wasio na changamoto kuendelea na uchaguzi kwa nafasi husika. Amesema kuwa Mara baada ya uchunguzi wa kina wa katika maeneo husika ,hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahusika kugombea na kisha kuwakabidhi katika vyombo vyenye dhamana ya kufuatilia masuala ya rushwa. “Mikoa ambayo tumefanya  uamuzi ni pamoja na kufuta uchaguzi wa umoja wa Vijana mko

RAIS SAMIA AMETOA SHILINGI BILIONI 1.5 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA CHUO.

Image
  Na Winner Marawiti MTENDAJI Mkuu wa Wakala  wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM),Dokta Siston Mgullah amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya chuo ambapo ukamilikaji wake utaboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Dokta Mgullah amesema hay oleo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023. Aidha ametaja vipaumbele vyao katika mwaka wa fedha wa 2022/2023,kuwa ni pamoja na kuandaa muongozo wa utawala bora kwa viongozi wa serikali za mitaa . Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema serikali imeweka fedha nyingi kwenye sekta ya elimu nchi nzima ambapo katika mwaka 2022/2023 kiasi cha Shilingi Trilioni 5.8 kimetengwa katika sekta ya elimu. Chuo cha ADEM kina majukumu mblaimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa viongozi na watendaji  wa elimu katika ngazi zot