RAIS SAMIA AMETOA SHILINGI BILIONI 1.5 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA CHUO.

 


Na Winner Marawiti

MTENDAJI Mkuu wa Wakala  wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM),Dokta Siston Mgullah amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya chuo ambapo ukamilikaji wake utaboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

Dokta Mgullah amesema hay oleo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Aidha ametaja vipaumbele vyao katika mwaka wa fedha wa 2022/2023,kuwa ni pamoja na kuandaa muongozo wa utawala bora kwa viongozi wa serikali za mitaa .

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema serikali imeweka fedha nyingi kwenye sekta ya elimu nchi nzima ambapo katika mwaka 2022/2023 kiasi cha Shilingi Trilioni 5.8 kimetengwa katika sekta ya elimu.

Chuo cha ADEM kina majukumu mblaimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa viongozi na watendaji  wa elimu katika ngazi zote na kufanya tafiti katika maeneo ya uongozi na usimamizi wa elimu ili kubaini na kutafuta ufumbuzi wake kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya elimu.


Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.