TAASISI ZA HAKI ZA BINADAMU ZITAMBULISHWE KWA WANANCHI.




Katika jitihada za kupambana na Rushwa na uvunjifu wa maadili na Haki za Binadamu,serikali imezitaka Taasisi zote nchini ambazo zinahusika na wajibu wa kuhakikisha Haki za Binadamu zinatambuliwa na 

kupatikana watimize wajibu wao wa kisheria katika kuwahudumia wananchi kwa weledi pamoja na kubuni njia na mbinu mbali mbali za kuwawezesha wananchi wafaidi Haki zao za Msingi.


Pichani: Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Prof. Ibrahimu Hamis Juma.


Akitoa Taarifa yake katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa Jijini Dodoma,Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Prof. Ibrahimu Hamis Juma amesema Usimamizi wa Maadili, Utawala Bora, na Vita dhidi ya Rushwa ni baadhi ya mbinu ambazo hutumika kuongeza, kuboresha na kustawisha upatikanaji wa Haki za Binadamu hapa nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akawataka wanachi kushiriki kutoa taarifa za uvunjifu wa maadili na haki za Binadamu kwa serikali ili kuweza kuimarisha Utawala Bora Nchini.

Awali akiwasilisha hotuba yake ,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Privatus Mizengo Pinda (Mb) amelaani vikali vitendo vya ukatili wa kina mama na watoto na kusema kuwa serikali haitokuwa na huruma kwa mtu yoyote atakaye bainika kufanya vitendo vya ukatili.

Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu limeainisha Haki na Uhuru ambazo kila mwananchi anastahili kuzipata bila kujali vigezo vya uraia wa nchi, sehemu unayoishi, jinsia, utaifa, asili yako, dini yako, lugha yako au hadhi yako yoyote.



Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.