WIZARA YA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI WATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA DODOMA
Pichani: Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Aloyce Muogofi akifungua kikao kazi cha mafunzo ya matumizi ya anuani za makazi kwa wafanyabiashara Jijini Dodoma.
Na Winner Marawiti,Dodoma
WIZARA ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imetoa mafunzo kwa wafanyabiashara mbalimbali wa Jijij la Dodoma kuhusu matumizi ya anuani za makazi lengo likiwa ni kuelewa utekelezaji wa mfumo huo kuelekea uchumi wa Kidijitali.
Akifungua Kikao kazi hicho Jijini Dodoma Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Aloyce Muogofi amesema kuwa kundi hilo la Wafanyabiashara ni kundi la kimkakati hivyo ni vyema sasa kuwa kidijitali katika ufanyaji kazo zao kama hitaji la Dunia linavyotaka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari,Mawasilinao na teknolonjia ya habari,Mhandisi Clarence Ichwekeleza amesema kuwa wameamua kutoa elimu hiyo kutokan na wafanyabiashara kuwa wengi na kukutana na watu wengi hivyo kupitia elimu hiyo watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine.
Awali akitoa wasilisho kuhusiana na anuani za makazi Muwezeshaji toka Wizara ya Ardhi,Nyumba na amendeleo ya makazi Anold Mkude amesema kuwa kama nchi Dunia inahitaji kuwa na anuani za makazi kutokana na Tanzania kuwa mwanachama wa umoja wa mataifa wa anuani za makazi.
Comments
Post a Comment