Posts

Showing posts from January, 2023

MABORESHO YA BANDARI YA TANGA KUONGEZA TIJA YA AJIRA NCHINI.

Image
  mwandishi wetu  Kutoka Tanga.  Maboresho ya Bandari ya  Tanga yanayofanywa na serikali  yanatarajiwa kuongeza uwezo wa Bandari ya Tanga kupokea mizigo kutoka Tangi 750,000 kwa mwaka hadi tani 3 milioni. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Bandari ya  Tanga Masoud Mrisha wakati akizungumza na waandishi wa habari za uchumi na biashara wanawake. alisema kutokana maboresho hayo mapato ya serikali na ajira zimeanza kuongezeka. Naye  meya wa Jiji la Tanga Abdulraman Shiloo alisema upanuzi huo pia unatarajia kuongeza  mapato kwa jiji la Tanga. Amesema maboresho hayo yamesababisha kuongezeka kwa shehena za mizigo jambo lililochangia upatikanaji wa mapato ambayo sehemu ya mapato hayo yamewezesha upatikanaji fedha katika jiji. " Tunashukuru maboresho haya yametupatia pesa ambayo ni sehemu ya asilimia kumi ya  mapato ya Halmashauri na pesa hiyo tumeikopesha kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu. Akizungumza na wanahabari hao mmoja wa wanufaika wa upanuzi wa mradi huo Bi Mwana