MABORESHO YA BANDARI YA TANGA KUONGEZA TIJA YA AJIRA NCHINI.
mwandishi wetu
Kutoka Tanga.
Maboresho ya Bandari ya Tanga yanayofanywa na serikali yanatarajiwa kuongeza uwezo wa Bandari ya Tanga kupokea mizigo kutoka Tangi 750,000 kwa mwaka hadi tani 3 milioni.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha wakati akizungumza na waandishi wa habari za uchumi na biashara wanawake.
alisema kutokana maboresho hayo mapato ya serikali na ajira zimeanza kuongezeka.
Naye meya wa Jiji la Tanga Abdulraman Shiloo alisema upanuzi huo pia unatarajia kuongeza mapato kwa jiji la Tanga.
Amesema maboresho hayo yamesababisha kuongezeka kwa shehena za mizigo jambo lililochangia upatikanaji wa mapato ambayo sehemu ya mapato hayo yamewezesha upatikanaji fedha katika jiji.
" Tunashukuru maboresho haya yametupatia pesa ambayo ni sehemu ya asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri na pesa hiyo tumeikopesha kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Akizungumza na wanahabari hao mmoja wa wanufaika wa upanuzi wa mradi huo Bi Mwanaidi Salim amepongeza na kushukuru kwa kupata ajira ya muda katika mradi kwani umemuwezesha kujiongezea kipato katika familia kwa kusaidiana na mwenzi wao katika kutekeleza majukumu ya familia Kama kulipa Kodi na kununua mahitaji ya shule kwa watoto wake.
Mwanaidi Salimu aliongezea kwa kusema dhana ya kwamba wanawake wa Tanga ni wavivu haipo tena kwani kwa Sasa wanawake wanafanya kazi.
Comments
Post a Comment