BODI YA BONDE LA MTO RUVU KUJENGA ZAIDI YA VISIMA 10 KUNUSURU ADHA YA MAJI.
Katika kutekeleza Mpango mkakati wa Majukumu mbalimbali ya Bodi ya Maji Bonde la Mto Ruvu imepanga kujenga zaidi ya Visima 10 katika mikoa ya Morogoro na Pwani ili kubakabiliana na changamoto za maji zinazokumba maeneo hayo.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibarik Mmasi wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu yanayofanywa na Bodi hiyo na kusema wamekuwa wakitoa vibali kulingana na mahitaji huku wakisimamia vyanzo vya maji kwa maendleo endelevu.
Aidha amesema bodi hiyo imekuwa ikidhiti utoaji maji taka katika viwanda ili kuyaboresha maji hayo yatumike kwa matumizi mengne na kuepukana na uchafunzi wa mazingira sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji .
Pia amebainisha mafanikio yaliyofanywa na bodi hiyo ikiwemo kukarabati na kuboresha miradi sugu ya visima vilivyoanzishwa kwa muda mrefu.
Hata hivyo ameitimisha kwa kutoa rai kwa watu wanaochimba visima holela na kuwataka wanachi kutoa taarifa ya visima hivyo ili kuepuka madhara yanayojitokeza kutokana na maji yasiyopelekwa maabara kufanyiwa vipimo.

Comments
Post a Comment