DOLA 88.4 KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI MANISPAA YA IRINGA

Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji  na usafi wa mazingira mkoa wa Iringa IRUWASA mhandisi David Palanjo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
 

Winner Marawiti, Dodoma

Katika kuhakikisha wananchi wanaepukana na adha ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini serikali imepanga kutekeleza mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika manispaa ya iringa utakao gharimu Dola za kimarekani 88.4.


Hayo yameelezwa leo hii Aprili 27,2023 na Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji  na usafi wa mazingira mkoa wa Iringa IRUWASA mhandisi David Palanjo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanukio, mikakati na changamoto za malaka hiyo. 


Aidha Mhandisi Palanjo amesema  mradi huo unatarijiwa kuanza mwezi Mei 2023 kwakufanya upembuzi na ujenzi kuanza April 2024 na kukamilika 2027 ambapo kutajengwa mtambo wa kusukuma maji lita milioni 6 kwa siku katika mji wa kilolo. 


Sambamba na hilo Mhandisi huyo amebainisha mafanikio yatokanayo na mamlaka hiyo kuwa ni pamoja na kuvuka lengo la sera ya maji ya ilani ya chama tawala kutaka kutaka kufikia asilimia 95% ya huduma kwa wananchi na badalayake wamefikia asilimia 97% na kuongeza idadi ya wateja  kutoka elfu 28,133 hadi elfu 40, 549 kwa mwaka 2022.



'Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imevuka lengo la sera ya maji na ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kutaka kufikia asilimia 95 kutoa huduma ya usambazaji Maji huku Mamlaka ikivuka lengo hilo kwa  kufikisha asilimia 97 na muda wa upatikanaji wa  maji ukiwa  wastani wa saa 23 kwa siku''.Mhandisi Palanjo


Kwa Mujibu  wa tafiti za Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na Maji (EWURA) katika kipindi cha miaka mitatu  IRUWASA imekua nafasi ya tatu kwa kutoa huduma bora za maji na kusimamia vizuri fedha zinazoelekezwa na Serikali katika  kutekeleza miradi mbalimbali ya maji Iringa.


"Miradi hii imetekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19 na imekamilika kwa asilimia 100 ikinufaisha jumla ya watu 15,398, kadhalika mradi wa maji wa Isimani Kilolo ulianza kutekelezwa Aprili, 2020 kwa njia ya force account kwa makadirio ya gharama ya Shilingi 9,270,306,365". Alisema 


Hadi mwezi Desemba, 2022, mradi wa Isimani-Kilolo ulikuwa umetekelezwa kwa asilimia 82 na jumla ya vijiji 20 kati ya 29 vinapata maji kwa sasa. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2023. Aidha, kati ya Shilingi 9,270,306,365, IRUWASA imeshapokea kiasi cha Shilingi bilioni 7.8 sawa na asilimia 84 ya gharama zote. 


 

"Mradi huu utakapokamilika, utaongeza uzalishaji wa maji kutoka lita 2,238,000 kwa siku hadi lita 4,656,000 kwa siku na hivyo kukidhi mahitaji kwa asilimia 100 na Wananchi watapata huduma ya maji kwa umbali usiozidi mita 400 na kila kituo kitahudumia wananchi wasiozidi 250 na wengine watapata huduma majumbani". Amesema Pallangyo 


Katika eneo la TEHAMA, IRUWASA imefanikiwa kwa kufunga mita za malipo kabla kwa wateja 6,752 na kuwa Mamlaka inayoongoza nchini kwa kufunga mita nyingi za maji za malipo kabla ambapo tangu mwezi Machi, 2016 Mamlaka ilianza kuzifungia mita za malipo ya kabla Taasisi za Serikali na wateja wa kawaida na wafanyabiashara ili kudhibiti ongezeko la madeni.


Hata hivyo inaelezwa Chanzo kikuu cha uzalishaji maji kwa Manispaa ya Iringa na maeneo ya pembezoni ni Mto Ruaha Mdogo na vyanzo vingine vidogo ni pamoja na chemichemi ya Kitwiru na visima vya viwili virefu vya Nyamhanga na Mawe.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.