TANZANIA YAFIKIA ASILIMIA 55 ZA KUPUNGUZA UGONJWA WA KIFUA KIKUU

Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Peter Neema Jijini Dodoma katika Uzinduzi.

 

Radia Abeid Khaji Mwakilishi wa Shirika la Shidefa Plus Kutoka Mkoani Shinyanga.

Na. Winner Marawiti

Kutoka Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema imefanikiwa kufikia  asilimia 55% za kupunguza ugonjwa wa Kifua Kikuu Nchini huku takwimu zikionesha kuwa maambulizi mapya yamepungungua kwa asilimia 32% kati ya 75% ambazo zililengwa  kufikiwa ifikapo 2025 ili kupunguza Vifo vitokanavyo na Ugonjwa huo.


Kauli Hiyo imetolewa na Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Peter Neema Jijini Dodoma katika Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Chini ya Awamu ya Sita Na Kusema wanafanya Mkakati wa kuongeza Mashine,Maabara na kutoa elimu kwa Ajili ya kupima Vina Saba vya Kifua Kikuu ili kufikia lengo la Uibuaji wa Ugonjwa huo.


Aidha wanatarija kufanyia maboresho katika Mpango Mkakati wa Sita ili kuchukuaa hatua zilitolewa katika ripoti ili kuwezesha kufikia malengo ifikapo 2025.


''Sasa hivi tunategemea kufanyia maboreshi katika mpango mkakati wetu wa sita ili kuchukua reccomendation zilizotolewa katika ripoti ili tuweze kufikia malengo yetu vizuri utakapofika mwisho wa mpango mkakati huu 2025''Dkt Peter.


Katika hatua nyingine Dkt.Peter amesema kumekuwa na changamoto kwenye uibuaji wa maambukizi mapya ya Kifua Kikuu ,kutokana wagonjwa wengi kukosa elimu bora  juu ya Uibuaji wa gonjwa Hili.


Kwa Upande wake Radia Abeid Khaji Mwakilishi wa Shirika la Shidefa Plus Kutoka Mkoani Shinyanga amesema wanatumia wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kwenda kutoa Elimu Juu ya Kifua Kikuu pamoja na kufanya uchunguzi wa awali kwa wachimbaji wa Madini wenye dalili za Ugonjwa huo ili kupelekwa kufanyiwa uchunguzi zaidi katika vituo vya Afya .


Comments

Popular posts from this blog

HUAWEI AIMS TO USE ITS  “4T”  TECHNOLOGIES TO ENABLE AN ENERGY LANDSCAPE TRANSITION OF 'FROMENERGY CONSUMER TO SUSTAINABLE ENERGY PRODUCER AND ENABLER'

WADAU WA MASUALA YA MAAFA WAJA NA MIKAKATI MADHUBITI YA KUDHIBITI MAAFA

RESHAPING INDUSTRIES WITH AI:HUAWEI CLOUD LAUNCHES PANGU MODELS 3.0 AND ASCEND AI CLOUD SERVICES