MH. SENYAMULE AZINDUA POLISI JAMII CUP DODOMA.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule katikati mwenye nguo ya blue akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ulinzi na Usalama na baadhi ya wachezaji kwenye uzinduzi wa ligi ya POLISI JAMII CUP DODOMA.
Na. winner Marawiti,Dodoma.
Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule, leo 24/2/2023 amezindua mashindano ya mpira wa miguu Polisi Jamii Cup yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mako Makuu katika Uwanja wa Shule ya Msingi central Jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule amewataka wananchi,pamoja viongozi kuanzia ngazi ya kijiji kushirikiana na jeshi la polisi kupitia mradi wa polisi Kata kutoa taarifa za wahalifu kwa Jeshi La Polisi na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Mh.Rorosemary amewasistiza wananchi kuwatumia vizuri polisi Kata walio katika maeneo yao ili kuweza kutatua migogoro na kutokomeza uhalifu kupitia elimu inayo tolewa na jeshi la polisi kwenye vikao na mikutano ili kuilinda amani ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu Polisi Jamii Nchi Cp Faustine Shigolile amesema lengo la kunzishwa kwa mashindano haya na jeshi la polisi ni kuifanya jamii hususani vijana kuepukana na vitendo vya kihalifu vinavyoenda kinyume na maadili.
Cp Shigolile amebainisha miradi ya Polisi jamii iliyo anzishwa na Jeshi la polisi ikiwemo mradi wa polisi Kata, mradi wa kuzuiya na kupambana na rushwa, kilimo na ufugaji pamoja na mradi wa huduma bure kwa mteja.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Acp Martin Otieno ameshukuru Jeshi La Polisi kwa kushirikiana na makao makuu kwa kuandaa mashindano hayo kufanyika kitaifa katika mkoa wa dodoma huku akiwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo na kupata elimu ya mapambano dhidi vitendo vya uhalifu, na ulinzi binafsi itakayo kuwa ikitolewa.
Comments
Post a Comment