SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

 


Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao kazi cha kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura kilichofanyika tarehe 16 Februari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha kujadili Rasimu ya Mapango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura wakiwa katika kazi za vikundi wakiujadili mpango huo.

 

Kamishna Msaidizi wa Polisi Makao Makuu Dodoma ACP Simon Haule akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa (Kituo cha Operesheni na Mawasilino ya Dharura) Bw. Prudence Constantino (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Mawasiliano ya Simu Wizara ya Habari, Mawasilino na Teknolojia ya Habari Mhandisi Edith Turuka wakifuatilia kikao hicho.

 

Mjumbe wa kikao cha wadau wa kupitia rasimu ya Mpango wa Taifa ya Mawasiliano ya Dharura Meja Lusajo Basyagile akichangia jambo wakati wa kikao hicho.


Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Yona Benjamin akiongoza kikao hicho.

 


Meneja Usimamizi wa Rasilimali za Mawasiliano na Tekinolojia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Felician Mwesigwa akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Taifa ya Mawasiliano ya Dharura wakati wa kikao cha kuupitia mpango huo Jijini Dodoma.

 


Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau cha kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura kilichofanyika tarehe 16 Februari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma.





Kutoka Dodoma.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kuweka mikakati madhubuti katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha inapunguza madhara yatokanayo na maafa.

Kauli hiyo imetolea na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge wakati akifungua kikao kazi cha wadau cha kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura kilichofanyika tarehe 16 Februari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma.

Kikao kazi hicho kililenga kupitia na kujadili rasimu ya mpango huo wenye malengo ya kusimamia mawasiliano na kuweka utaratibu wa matumizi ya huduma za mawasiliano ndani ya Serikali, Umma, Wadau wa Mawasiliano na Mashirika Binafsi.
 
Meja Jenerali Mbuge alisema, upo umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wote wa masuala ya maafa nchini kwa lengo la kuhakikisha wanaendelea kuwa na mikakati madhubuti ya mawasilino wakati wa dharura.

“Hakikisheni kuwa mpango unazingatia Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022, Kanuni za Usimamizi wa Maafa za mwaka 2022 na Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa Maafa 2022 ili kurahisisha utekelezaji wake,”alisisitiza Meja Jenerali Mbuge.

Akieleza kuhusu Mpango huo, alisema utarahisisha mawasilino ya haraka, sahihi na kwa wakati unaohitajika kwa kuzingatia mfumo huo uliojikita kidijiti na unahusisha vyombo vya habari ikiwemo matumizi ya radio, televisheni na mitandao ya kijamii.

Katika hatua nyingine Idara imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa kuhakikisha usimamizi na uratibu wa maafa na huduma za dharura zinatolewa kwa wakati kwa kuzingatia mipango, miongozo na mikakati ya kitaifa na kisekta. Juhudi hizi zimekuwa zikifanyika kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi, Mashirika ya kimataifa na Asasi zisizo za kiserikali.

“Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Na. 6 ya mwaka 2022 inajukumu la kuratibu na kusimamia masuala ya maafa nchini,”alisema.

Idara ya maafa ilizindua nyaraka za usmamizi wa maafa nchini ikiwemo; Mkakati wa Taifa wa
Mawasiliano ya Dharura 2022 ambao umelenga kuhakikisha utendaji kazi, ushirikiano, na mwendelezo wa mawasiliano vinaimarika wakati wa maafa ili kuruhusu watoa huduma za dharura kufanya mawasiliano baina yao na ngazi nyingine za serikali wakati wote, hata pindi miundombinu ya mawasiliano itakapoharibiwa.

Comments

Popular posts from this blog

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.