TANESCO KUZALISHA MEGEWATI 5000 ZA UMEME IFIKAPO MWAKA 2025

 GU6A0408

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Martin Mwambene akizungumza na wanahabari jijini dodoma.

Na Winner Marawiti.


kutoka DODOMA


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Martin Mwambene amesema hadi kufikia mwaka 2025 Shirika hilo litakuwa limefikia malengo ya uzalishaji wa Megawati 5000,kutokana na miradi kadhaa ambayo inachangia kuongeza uzalishaji wa umeme katika gridi ya taifa kila mwaka.

 

Ameyasema hayo Jijini Dodoma leo Februari 23,2023,wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali ya shirika hilo na uelekeo wake kwa mwaka wa 2023 ,akiwa na waandishi wa habari.

 

 Aidha amesema kuwa kwa sasa shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 1,820,wakati mitambo iliyopo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,300 pekee. 

 

 "TANESCO inafanya miradi kadhaa ambayo inasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka ambapo malengo ni kufikia Megawati 5000 ifikapo 2025,"amesema Mwambene 

 

Mwambene ameongeza kuwa TANESCO kwa kutambua matatizo ya umeme yaliyopo nchini imekuja na mradi wa Gridi Imara ambapo katika bajeti ya mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake.

 

 Katika mradi wa Grid Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6000,mita laki 7za umeme, nguzo 380,000,ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa km 40,000, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takribani kilomita 948 na ujenzi wa vituo 14 vya kupooza umeme. 

 

Kaimu Mkurugenzi huyo amezungumzia pia maendeleo ya ujenzi katika Bwawa la Mwalimu NYerere kuwa upo katika asislimia 88 na zoezi la uwekaji maji limefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.