TBA YATEKELEZA MAAGIZO YA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT SAMIA SULUHU HASSAN.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Ndug. Daud Kondoro akizungumza na waandisi wa habari jijini dodoma.

Winner Marawiti,

Kutoka DODOMA.

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Ndug. Daud Kondoro amesema kuwa TBA imetekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.,Samia Suluhu Hassan kuhusu bei za nyumba za Magomeni Kota,Jijini Dar es Salaam.


Mtendaji Mkuu huyo ameeleza haya Jijini hapa ,Februari 14,2023, wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo kwa mwaka 2021-2022 na 2022-2023.


Kondoro ameeleza kuwa baada ya maagizo ya Rais walikutana na timu ya watalaamu na blogana namna ya kufunga bei ya nyumba hizo.


Ambapo amesema kutokana na maelekezo ya Rais wameweza kuondoa shilingi bilioni 18.2 na kwa sasa bei ya nyumba ya chumba kimoja itauzwa kutoka Shilingi Milioni 74.8 hadi Shilingi milioni 48 na ya nyumba mbili kutoka Shilingi milioni 86 hadi Shilingi milini 56.9.


“Hii ni kutokana na gharama ya nyumba hizi kwa kuondoa gharama za ardhi,maeneo juu kama korido, mandhari ya nje,mashimo ya maji taka na vizimba vya ngumu vilivyokuwa vimepokea awali"


Aidha amesema imekubaliana kuwa deni litarudishwa kwa miaka 15 na miaka 5 watakaa bure lakini hakutakuwa na riba.


“Niseme hakuna sakata kwa upande wa wakala tunatambua umoja wa wanakota,”amesisitiza.


Machi 23 mwaka jana Samia wakati akizindua nyumba hizo aliutaka Wakala gharama gharama za matumizi ya nyumba hizo kwani zipo juu.


Awali nyumba hizo zilikuwa zikiuzwa kwa Sh74 milioni kwa chumba na sebule na Sh86 milioni kwa vyumba viwili na viwili.


Februari 6 mwaka huu wakazi 644 wa Magomeni Kota waligomea kusaini mkataba wa kuanza kununua nyumba hizo, kwa madai kwamba bei waliyoletewa sio rafiki na haiendani na hali ya uchumi wao.


Akizungumzia utekeleza wa majukumu ya TBA kwa mwaka 2021/22 2022/23 Kondoro ametaja utekelezaji uliotekelezwa kwa fedha za ruzuku amesema kuwa TBA ilipokea jumla ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 54.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ikijumuisha Mradi wa Ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Dodoma.


Ametaja miradi mingine ni mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi jijini Dodoma,Ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Umma katika eneo la Magomeni Kota, awamu ya kwanza na ya pili,Ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Temeke Kota ambapo linajengwa jengo la ghorofa 9 linalochukua familia 144.


“Ujenzi wa nyumba tano za majaji katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro, Mtwara, Kagera na Shinyanga, ambapo nyumba nne zimeshakamilika na kuanza, Ujenzi wa nyumba ya jaji Kagera unaendelea na umefika 30% ya utekelezaji Ukarabati wa nyumba 40 za viongozi. jijini Dodoma, awamu ya kwanza na ya pili, Ukarabati wa nyumba 30 jijini Dar es Salaam,Ukarabati wa nyumba 66 za iliyokuwa mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), pamoja na Ukarabati wa nyumba katika Mikoa 20 zilizohamishiwa TBA kutoka TAMISEMI.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.