TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU)kupitia wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia imeweka utaratibu wa kuanzishwa na kuimarishwa Mifumo ya uthibiti ubora ndani ya vyuo vikuu ambapo vyuo vyenyewe vimekuwa na utaratibu wa kujikagua, kujitathmini na kufanya Marekebisho mbalimbali kwa kuzingatia Miongozo ya uendeshaji wa vyuo vikuu nchini.
Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa shughuli Mbalimbali za Tume hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita leo JIJINI Dodoma, katibu Mtendaji wa tume Prof Charles kihampa amesema mifumo ya ushauri,ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara imefanya vyuo kufanya maboresho makubwa katika miundombinu ya Kufundishia na kujifunzia.
Aidha, prof Kihampa amesema Tume ya vyuo vikuu imeendelea kuimarisha Mifumo yake ya uthibiti ubora na Mifumo ya ndani ya vyuo vikuu ili kuhakikisha vyuo vikuu vinaendana na mwelekeo wa nchi.
Sambamba na hayo Prof kihampa ameongeza kuwa serikali imeendelea kutekeleza kwa Vitendo azma yake ya kuongeza wigo wa fursa za masomo ya Elimu ya juu kwa watanzania ambapo katika vyuo vya Elimu ya juu katika programu za shahada ya kwanza zimeongezeka kama anavyoeleza.
Dhamira ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) ni kuhakikisha uwepo wa Mifumo endelevu ya Elimu ya ngazi ya chuo kikuu ili kupata wahitimu wenye Elimu, Maarifa,ujuzi na uwezo wa kustahimili ushindani Kitaifa,kikanda na Kimataifa.
Comments
Post a Comment