VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZINAZOTOKANA NA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO(e_GA).

 

Mhandisi Benedict B.Ndomba Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya serikali mtandao(e_GA) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma


Na.Winner Marawiti.

Dodoma.



Vijana wakitanzania wameaswa kutumia fursa zinazotokana na mamlaka ya serikali mtandao (e_GA) kwani kupitia mamlaka hiyo wanaweza kuonesha bunifu zao na kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya tehama ili kuendana na kasi ya kidijiti.

Hayo yamesemwa na Mhandisi Benedict B.Ndomba Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya serikali mtandao(e_GA) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelezea utekelezaji wa majukumu ya mamlaka ya serikali mtandao (e_GA).

"Tunafanya kazi kwa karibu na COSTECH pamoja na vyuo vya elimu ya juu ili kuweza kuwasaidia vijana lakini pia tunawafundisha nini haswa kinachohitajika kwenye fursa zinazotokana na ubunifu wa tehama"Amesema Mhandisi Ndomba.

Aidha amesema mamlaka inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi yake mikuu sita(6) ambayo ni uadilifu,ubunifu,kuthamini wateja,kufanya kazi kwa pamoja,ushirikiano na weledi.


Ameongeza majukumu mengine ni kuzijengea uwezo taasisi za umma kutekeleza jitihada za serikali mtandao, taasisi mbalimbali za umma zimewezeshwa kutekeleza jitihada za serikali mtandao kwa kutoa mafunzo mbalimbali kama vile usimamizi wa mtandao wa mawasiliano wa serikali kwa taasisi 240,kutoa mafunzo ya mfumo wa Baruapepe kwa taasisi 611 kutoa mafunzo ya usimamizi wa tovuti kwa taasisi 492.

" Kupitia na kupitisha miradi ya TEHAMA ya taasisi za Umma katika kipindi hiko miradi 340 imepitiwa na kuthibitisha"Amesema Mhandisi Ndomba.

Mamlaka inashirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi zikiwemo taasisi za elimu ya juu na utafiti,sekta binafsi pamoja na kuandaa vikao kazi vya mwaka vya serikali mtandao ili kuwakutanisha wadau mbalimbali ambapo katika kikao kazi kinachofanyika februari mwaka huu jumla ya washiriki 1,624 walihudhuria ambao ni wakuu wa Taasisi za umma,wataalamu wa TEHAMA na watumiaji wa Tehama katika taasisi za umma.

Aidha mamlaka inashirikiana na wakala ya serikali mtandao Zanzibar(e_GAZ) kwa lengo la kuhakikisha serikali mtandao inaimarika kote Bara na visiwani kupitia ushirikiano huu mifumo kadhaa imeboreshwa na inatumiwa na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) mifumo hii ni pamoja na mfumo wa barua pepe serikalini,mfumo wa masjala,mfumo wa malipo Zanzibar (Zanmalipo) mfumo wa ajira (ZanAjira) e_wawakilishi na mfumo wa Ankara za maji (MAJIIS) kwa ajili ya mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) pia mamlaka inashirikiana na EGAZ katika utoaji wa huduma ya miundimbinu ya serikali mtandao.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.