WATANZANIA PATENI ELIMU YA MIKOPO

 



 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa akizungumza na Wanahabari Jijini Dodoma Februari 13,2023.


winner Marawiti

Kutoka Dodoma

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa amesema kuwa Watanzania wengi bado hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha itokanayo na mikopo na badala yake wanakopa na kutumia nje ya mipango waliyokusudia.

Ameyasema haya Jijini Dodoma, leo Februari 14,2023 wakati akizungumz na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo.

Aidha Beng’i ameeleza kuwa pamoja na Serikali kutoa fedha za mikopo kiasi cha shilingi Trilioni 5.6 kwa ajili ya kuwawezesha watanzania milioni 8 bado watanzania wengi wanakabiliwa nakutokua na elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Nataka kuwaeleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana baraza kwa kushirikiana na serikali kwa ujumla wake wametoa kiasi cha sh.tirion 5 .6 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wapatao milioni 8 jambo ambalo ni hatua kubwa katika kuwawezesha watanzania kujiinua kiuchumi”.

Kutokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha amesema kuwa serikali kwa kushirikiana taasisi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa watanzania ili kuhakikisha watanzania wanajikwamua katika maisha na kuishi maisha ambayo yatakuwa bora kila mmoja jambo ambalo litawafanya watanzania kuwa na amani na furaha”.

Pamoja na hayo Beng’i amewashauri watanzania kutopenda kujitumbukiza kwenye masuala ya mikopo kama hawajajipanga kwa kujua wanachotakiwa kukifanya.Aidha amewataka watanzania kuwa na nidhamu ya fedha sambamba na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba benki.

Vilevile amezungumzia ufanisi wa baraza hilo ambapo amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kihuchumi .

Katika kutilia mkazo juu ya kuwawezesha wananchi ameeleza kuwa kwa sasa kuna mifuko mbalimbali ya kuwawezesha akina mama na vijana huku akieleza kuwa akina mama wamekuwa wakipewa kipaumbele zaidi kwa kuwa ni waaminifu katika kurejesha.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.