WAZIRI MKUU AZITAKA SERIKALI ZA MITAA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MAAFA






Na.Winner Marawiti

Kutoka Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim amezitaka Wizara, Taasisi na Tawala za Serikali za Mitaa kutenga fedha kwa ajili ya Utekelezaji wa Shughuli za Maafa katika maeneo yote kwa kuzingatia bajeti ya mwaka 2023/24.


Maelekezo hayo yametolewa Jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Hafla ya Nyaraka za Usimamizi wa Maafa huku akiwataka wananchi kuwa sehemu ya Utendaji katika shughuli za Maafa yanayojitokeza.


Aidha ametoa wito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuimarisha Vikundi vya Skauti kutoka shule za Msingi mpka Sekondari zilizopo chini ya Mamlaka hiyo ili kuwajengea uwezo ,ukakamavu na ari ya kujitoa katika kukabiliana na Majanga mbalimbali.


Kwa upande wake Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Sera,Bunge na Uratibu Geogre Simbachawene ametoa rai kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari mapema kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.


Uzinduzi wa Nyaraka hizo Utasaidia katika upatikanaji wa Taarifa za Maafa kwa wakati na kuwezesha wahusika kuchukua hatua haraka.



Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUMBARO AMEWATAKA VIONGOZI WA TAASISI ZA UTOAJI HAKI KUSHIRIKIANA KATIKA KUONDOA VIKWAZO VINAVYOKWAMISHA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA WATOA TAARIFA

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.