WCF KUBORESHA HUDUMA MUHIMU KWA WADAU NCHINI KWA NJIA YA MTANDAO
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa CHF Dkt.John Mduma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mfuko huo leo Machi 2,2023, Jijini Dodoma
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi {WCF} imeendelea kuboresha, kuhakikisha huduma muhimu kwa wadau nchi nzima kwa njia ya mtandao kufikia malengo ya Mfuko huo.
Huduma hizo za kimtandao ni pamoja na Usajili wa wanachama ambapo Mwanachama wa Mfuko huo ni Waajiri, kupata cheti cha Usajili,kuwasilisha michango kila mwezi,Mfuko unnapokea mchango kupitia nambari ya Udhibiti ambayo hupatikana kwa njia ya Mtandao.
Hayo yamebaishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt.John Mduma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mfuko huo leo Machi 2,2023, Jijini Dodoma na kusema hadi kufikia Juni 30 2022 Mfuko umekusanya kiasi cha Shillingi Bilioni 241.48 ikiwa ni kutokana na mapato ya uwekezaji.
"Hadi kufikia tarehe 30 June 2022,Mfuko umekusanya jumla ya Shillingi Billioni 241.48 toka kwenye mapato yanayotokana na uwekezaji" Amesema Dkt. Mduma.
Aidha amesema kuwa kabla ya kuanzishwa kwa WCF malipo ya fidia nchini kwa mwaka mzima yalikuwa chini ya Shillingi millioni 200 lakini baada ya kuanzishwa kwa Mfuko huo malipo yanaongezeka kila mwaka.
"Mfuko huu umekuwa na faida kubwa kwani lengo,lake kubwa ni kuwakomboa wafnykazi waliopata madhili ama majanga wakiwa kazini kutoka katika dimbwi la umasikini ambapo takwimu za hivi karibuni zikionesha tangu kuanzishwa, idadi ya wanufaika wa Mfuko imefikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya shilingi Billioni 49.44,"amesema Dkt.Mduma.
Katika hatua nyingine,Dkt.Mduma amesema kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2021 hadi Februari 2023 Waajiri wapya 5,250 wamejisajili WCF huku kati ya waajiri hao asilimia 99.27% ni waajiri wakubwa ,huku asilimia 98.71% ni waajiri wa kati na waajiri wa chini ni asilimia 88.56%.
"Waajiri wengi kwa sasa wanavutiwa kujisajili na WCF kutokana na Serikali sikivu ya awamu ya sita kupunguza kiwango cha mchango kwa sekta binafsi kutoka asilimia 1 ya hapo awali kabla ya maboresho ya kisera hadi asilimia 0.5 ya sasa hivyo kuleta mlingano wa michango kuwa sawa na sekta za umma,"
Na kuongeza kuwa "Lakini serikali pia imeendelea kuleta unafuu kwa waajiri kwa kupunguza kiwango cha kodi ya malimbikizo ya madeni ya michango ya nyuma kutoka asilimia kumi (10%) hadi asilimia mbili (2%)
Hata hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la waajiri kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi {WCF} katika kipindi cha Awamu ya Sita.
Comments
Post a Comment