JWTZ LATANGAZA NAFASI ZA KUJIUNGA NA JESHI KWA VIJANA WA KITANZANIA

kaimu mkurugenzi wa Habari na uhusiao wa JWTZ, Luteni Kanali GAUDENTIUS ILONDA akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Leo Machi, 9,2023.

Na.Winner Marawiti,Dodoma.

 Jeshi la wananchi Tanzania limetangaza nafasi za kujiunga na jeshi kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidaato cha nne hadi shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba wa miaka miwili wa mafunzo ya kujitolea katika jeshi la kujenga taifa na kurudishwa majumbani.


Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari leo march 9 2023 Jijini Dodoma kaimu mkurugenzi wa Habari na uhusiao wa JWTZ, Luteni Kanali GAUDENTIUS ILONDA, amesema nafasi hizo zinawahusu vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu.


Aidha,Luteni Kanali ILONDA, ameeleza vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa katika maombi hayo kuwa mwombaji awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na akili timamu,awe na cheti halisi cha kuzaliwa,vyeti vya shule nav yeti vya taaluma.


Vigezo vingine ni pamojana na awe hajatumikia Jeshi la Polisi,magereza,Chuo cha Mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo na asiwe ameoa au kuolewa.


Kwa upande wa utaratibu wa jinsi ya kutuma maombi Luteni Kanali Ilonda ,amebainisha kuwa maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya jeshi hilo Dodoma kwanzia leo tarehe 9,Machi hadi tarehe 20 ,Machi 2023 yakiwa na viambatanisho kama vile nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya nida,nakala ya cheti cha kuzaliwa,vyeti vya shule na chuo,nakala cheti cha JKT nan amba ya simu ya mkononi ya muombaji.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.