KANISA LA EAGT LAMKABITHI GARI ASKOFU MKUU MWAKIPESILE

 

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Brown Abel Mwakipesile wakati wa Hafla ya kukabidhiwa gari ya Utumishi na kanisa hilo Jijini Dodoma


Na.Winner Marawiti,Dodoma.

Katika kuazimisha siku ya Wanawake Duniani Kanisa la (EAGT) Dodoma limewataka wakina mama kutambua ratiba ,hasa katika majukumu ya kulea na kutunza watoto pamoja na waume zao kwa sababu mwanamke ndio wenye uchungu zaidi hivyo wanapaswa kuwa na wajibu wenye utaratibu wa kifamilia.


Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Brown Abel Mwakipesile wakati wa Hafla ya kukabidhiwa gari ya Utumishi na kanisa hilo Jijini Dodoma huku akiwaasa wanadamu kutopumbazika na utandawazi kwa sababu Misingi ya Mungu ipo wazi na inaelekeza namna Mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata mienendo ya Biblia.

''Mimi nasema wanadamu wasizuzuke kwa sababu Misingi ya Mungu ipo wazi Kibiblia Mungu aliweka utaratibu wa mwanadamu anapaswa kuishije kwa sababu kinachokuwa chema kina mipaka yake na mtu kama umeumbwa na utashi wa busara unapaswa kupambanua kipi kinafaa na kipi kisichofaa kwa ajili ya manufaa yake''amesema Dkt.Mwakipesile

Aidha Dkt. Mwakipesile amesema Kanisa la EAGT wanapambana kuubiri injili watu kuacha Uovu wabaki na mawazo waliyopewa na Mungu ili wapate kumuheshimu Mungu anapowapa afya na uzima.

''mambo ya ushonga,ulawiti ni kinyume na mapenzi ya Mungu na yataleta hukumu kubwa kwa wanadamu na hii italeta laana kubwa hata katika familia na jamii watanzania waepuke kuigiza sana vitu visivyofaa''amesema Dkt.Mwakipesile.

Kwa upande wake Makamu Askofu Mkuu (EAGT) Askofu. Joshua Wawa amesema Dkt. Mwakipesile amekuwa akijitaabisha kwa kazi ya Mungu kwanzia ngazi ya chini hadi majimbo hivyo kutokana na jitihada zake na kuzitambua kwa kazi anazozifanya ikawapasa wao kama kanisa kumnunulia chombo cha usafiri.

''Amekuwa akijitaabisha kwa kazi ya Mungu kwanzia ngazi ya chini hadi majimbo na kutokana na jitihada na kuzitambua kazi anazozifanya ikatupasa sisi kumnunulia chombo cha usafiri''amesema Askofu Wawa.

Hata hivyo amehitimisha kwa kusema kanisa imefanya hayo kwa ujulisho kwa kuwa ukitenda vyema kazi ya Mungu utaenziwa kuanzia Duniani
.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.