TASAC YATOLEA UFAFANUZI JUU YA UZUSHI WA VIJANA 209 WALIOFUTIWA MKATABA WA MAFUNZO KWA VITENDO KAZINI.

 

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bwana Kaimu Mkeyenge akitolea ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Kwenye ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma Machi 10,2023.


Na WINNER MARAWITI-DODOMA



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bwana Kaimu Mkeyenge ametolea ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan Twitter na Instagram kuhusu malalamiko dhidi ya Shirika hilo yanayosema kuwa Mikataba ya mafunzo kwa vitendo kwa vijana zaidi ya 400 waliokuwa TASAC ilivunjwa bila kufuata utaratibu na ikiwa imebaki muda wa mwaka mmoja kuisha kwa mikataba hiyo.



Mkeyenge ametoa ufafanuzi huo Jijini Dodoma Machi 10/2023 wakati akitoa taarifa kwa Umma kupitia waandishi wa habari kuhusu Vijana hao waliokuwa wanafanya shughuli za Mafunzo ya kazi ndani ya shirika hilo.



Bwn Mkeyenge amesema kuwa tuhuma walizotoa Vijana hao ni kuwa wanafanya kazi bila bima ya afya na kwamba TASAC ilitoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) katika mashauri ya kazi yaliyofunguliwa na vijana hao ili haki isitendeke.


''Hakuna sheria inayomtaka muajiri yeyote yule kumkatia bima ya afya kijana anayefanya shughuli za Mafunzo kazini suala hilo halipo na hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya hivyo kwani stahiki zao zimeainishwa kwenye Muongozo wa Kitaifa wa Mafunzo Kazi uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na tuhuma kuhusu TASAC kutoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili mashauri ya kazi yaliyofunguliwa na vijana hao haki isitendeke hakuna ukweli wowote''.


Pia Bwn Mkeyenge ameongeza kuwa kati ya vijana 209 waliofutiwa mikataba yao, ni vijana 41 tu ambao hawakuridhika na maamuzi hayo ambapo vijana 32 kati ya vijana 41, shauri lao lilifutwa na CMA kwa kuwa liliwasilishwa nje ya muda, hivyo ni vijana 9 tu ambao shauri lao dhidi ya TASAC lilipokelewa na lipo katika Tume ya Usuluhisi na Uamuzi.


Ambapo vijana 168 waliobaki hawakupinga uamuzi wa TASAC wa kuvunja mikataba yao kutokana na mabadiliko ya Sheria ambayo yalikuwa ni nje ya uwezo wa Shirika.


Mkurugenzi huyo amesema suala hilo lipo kwenye chombo cha maamuzi kisheria, TASAC haipaswi kuzungumzia shauri hilo ila waliona ni busara kulitolea ufafanuzi wa kilichofanyika kwa upande wa TASAC na kuacha hatua za maamuzi zinazoendelea kuchukua mkondo wake.


TASAC ni Shirika la Umma linalotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali, hivyo linatoa wito kwa Umma kuwa na subira wakati Tume inapoyafanyia kazi mashauri hayo.



Katika hatua nyingine amesema TASAC ni taasisi ya Serikali inayosimamiwa na Sheria, Kanuni na Miongozo ya Serikali, hivyo basi mashauri yake kisheria yanasimamiwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ikiwa ni pamoja na shauri hili hivyo kwa mantiki hiyo, Shirika hilo halijatoa na haiwezi kutoa rushwa yoyote kwa CMA ili kuzuia haki isitendeke kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii.


''Kwa mantiki hiyo, niwahakikishie kuwa TASAC haijatoa na haiwezi kutoa rushwa yoyote kwa CMA ili kuzuia haki isitendeke kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii'' amesema Bwana Mkeyenge


Hata hivyo Mkeyenge amehitimisha kwa kusema kati ya vijana 209 waliofutiwa mikataba yao, ni vijana 41 tu ambao hawakuridhika na maamuzi hayo Vijana 32 kati ya vijana 41, shauri lao lilifutwa na CMA kwa kuwa liliwasilishwa nje ya muda, hivyo ni vijana 9 tu ambao shauri lao dhidi ya TASAC lilipokelewa na lipo katika Tume ya Usuluhisi na Uamuzi.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.