WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA WIZARA YA AFYA KUONGEZA JITIHADA KWENYE MAGONJWA YA MLIPUKO

 

IMG-20230322-WA0121
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera ,Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene,akizungumza leo leo Machi 22,2023 ,Jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu wa mwaka 2023-2027 wenye kauli mbiu isemayo "Ushirikiano wa Kisekta ni mkakati sahihi wa kuzuia ,kukabiliana na kutokomeza kipindupindu nchini Ifikapo mwaka 2030,".
IMG-20230322-WA0126
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera ,Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene, akibonyeza kitufe katika kompyuta kuashiria uzinduzu mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu wa mwaka 2023-2027 wenye kauli mbiu isemayo "Ushirikiano wa Kisekta ni mkakati sahihi wa kuzuia ,kukabiliana na kutokomeza kipindupindu nchini Ifikapo mwaka 2030,".
IMG-20230322-WA0122
Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akizungumza leo Machi 22,2023 ,Jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu wa mwaka 2023-2027 wenye kauli mbiu isemayo "Ushirikiano wa Kisekta ni mkakati sahihi wa kuzuia ,kukabiliana na kutokomeza kipindupindu nchini Ifikapo mwaka 2030,".


Na Hamis mniha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera ,Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene, ameitaka Wizara ya Afya kuongeza ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu ili kuhakikisha unadhibitiwa usisambae nchini hususani katika maeneo ambayo yanapata milipuko ya mara kwa mara.

Mhe.Simbachawene ameyasema hayo leo Machi 22,2023 ,Jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu wa mwaka 2023-2027 wenye kauli mbiu isemayo "Ushirikiano wa Kisekta ni mkakati sahihi wa kuzuia ,kukabiliana na kutokomeza kipindupindu nchini Ifikapo mwaka 2030,".

"Sisi wote ni muhimu katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa huu wa kipindupindu ambapo chanzo chake kikubwa imeonekana kuwa ni matumizi ya maji yasiyo salama hivyo niwaombe wizara ya afya kuhakikisha wanapeleka nguvu katika maeneo yaliyoathirika sana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu,"amesema Mhe.Simbachawene

IMG-20230322-WA0125

Pia amezitaka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kushirikiana na Mamlaka za maji mijini na vijijini kuhakikisha wanadhibiti matumizi ya maji na kuhakikisha maji yanayotumika ni salama na kudhibiti pia Maji taka yasitiririke katika mazingira na makazi ya watu ili kuepukana na milipuko ya magonjwa ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu.

Hata hivyo ,ameitaka ofisi hiyo kuongeza kasi katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya vyoo bora,matumizi ya maji safi na salama ,kutotiririsha maji taka hovyo,kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla na baada ya kula ili kupunguza milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu.

IMG-20230322-WA0127

"kipindupindu ni ugonjwa wa aibu ambao haupaswi kutajwa katika nchi yetu ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Miundombinu na sekta zingine hivyo ni aibu sana kuendelea kuwa na tishio la ugonjwa huu wa aibu,"amesema Mhe.Simbachawene

Naye Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel amesema kuwa kwa mwaka 2015 Tanzania ilikuwa na visa vilivyoripotiwa vya ugonjwa wa kipindupindu 12,985 wakati kwa mwaka wa 2022 visa vilivyoripotiwa ni 537 na upungufu huo ni kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mh Dkt Samia Suluhu Hassan.

IMG-20230322-WA0124

"Tunawahakikishia wadau wetu kuwa wizara ya afya na Serikali kwa ujumla inatambua mchango wenu mkubwa mnaoutoa kuwasaidia watanzania katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu na tunaahidi kuwa kama kuna changamoto yeyote tutakwenda kuifanyia kazi ili nanyi muweze kutekeleza majukumu yenu vyema,"amesema Dkt Mollel

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Ukimwi Mhe.Elibariki Kingu amesema kuwa uzinduzi wa mpango huo serikali inalenga kuhakikisha inaondoa kabisa ugonjwa wa kipindupindu na ibaki kuwa historia.

IMG-20230322-WA0120

"Sisi ambao tunapata huduma zote zpmuhimu tunaweza kujikuta tunawasahau watu wa chini ila kwa mpango huu mnafanya kazi ya Mungu hivyo kamati inaahidi kushirikiana na nyinyi katika hili kuhakikisha ugonywa huu unatokomezwa na inabaki kuwa historia katika nchi yetu,"amesema Mhe.Kingu

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Save the Children Tanzania Angela Kauleni ,amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Januari mpaka machi mwaka 2023 shirika hilo kwa kushirikiana na waganga wakuu wa mikoa na wilaya wamefanikiwa kutoa mafunzo kwenye jamii ambapo watu 5000 wamepatiwa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu.


IMG-20230322-WA0123


Pia amesema changamoto walizokutana nazo ni pamoja na jamii ya wafugaji kutokukubaliana na elimu na kuendana na mabadiliko yaliyopo kwa sasa na baadhi ya jamii kuwa na mila potofu kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo wakiamini kuwa ni ushirikina.

"Jamii nyingi za wafugaji zimekataa kabisa kukubaliana na elimu pamoja na mabadiliko yaliyopo kwa sasa na wengine wamekuwa na imani potofu kuwa mlipuko wa ugonjwa huo ni ushirikina jambo ambalo sio kweli na hapa serikali inatakiwa iongeze kasi katika kuelimisha jamii kuhusu magonjwa haya ya mlipuko,"amesema Kauleni

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.