Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma akieleza mafanikio ya Baraza hilo katika  kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya  Awamu ya Sita.


Na.Winner Marawiti,Dodoma.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC} katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 limepokea na kushughulikia malalamiko takribani 369 ya Uchafuzi na Uharibifu wa Mazingira kutoka kwa wananchi ikiwemo kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya mafuta ,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria.


Hayo yameelezwa leo Machi 3,2023Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Samwel Gwamaka wakati akieleza mafanikio ya Baraza hilo katika  kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya  Awamu ya Sita.


 Ambapo Dkt.Gwamaka amesema malalamiko hayo yalihusisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, utiririshaji wa maji taka ,uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwandani,kelele za muziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi,kushamiri vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu,matumizi ya mifuko ya plastiki iliyokatwa na kutapaka maeneo ya makazi na kuhakikisha inatoa elimu elimu sahihi na suluhisho juu ya jambo husika.

Aidha Dkt Gwamaka amesema Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya {TAM} na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira.


"Kwa kupitia taarifa ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya {TAM} na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira" amesema Dkt.Gwamaka


Katika hatua nyingine Dkt.Gwamaka amebainisha kuwa  Baraza hilo limetoa Jumla ya Vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi ambapo vibali 10 vya kuingiza  na kusafirisha nje ya Nchi na kupelekea kiasi cha Tani 516,041 za taka mbalimbali kukusanywa na  makampuni yenye vibali.

 "kukusanywa huku kwa tani 516,041 inaonesha jinsi Braza linavyowajibika katika kuhakikisha  Sheria ya Mazingira inayozingatia uhifadhi na utunzaji wake unazingatiwa na ndio maana pia tumetoa jumla ya vibali  174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi yetu .


Hata hivyo amebainisha usimamizi wa tafiti za Mazingira huku ikifanikiwa kuratibu uteuzi wa Eneo la Rufiji-Mafia-Kibiti-Kilwa {RUMAKI} ikiwa na lengo la kujumuishwa katika mtandao wa kidunia wa Hifadhi za Binadamu na Hifadhi hai.

Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

HUAWEI ANNOUNCES SWITCH TO METAERP,REDEFINING ENTERPRISES 'CORE BUSINESS SYSTEMS

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.