TASAC KUKAGUA MELI 61 ZA KIGENI 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu Mkeyenge akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma.
Na Winner Marawiti.
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), imebainisha kuwa inatekeleza miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini yanazingatiwa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw.Kaimu Mkeyenge leo Machi 7,2023 Jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TASAC, pamoja na kubainisha Mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Na kuongeza kuwa "mifumo ya TEHAMA ulianza mwaka wa fedha 2018/19 na utakamilika mwaka wa fedha 2025/26 huku mifumo ambayo inayoboreshwa ndani ya Shirika ni pamoja na mfumo wa ukaguzi, usajili wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa vyeti vya Mabaharia (Maritime Administration Management System), mfumo wa utoaji leseni, ukusanyaji wa mapato ya udhibiti, uhakiki kadhia na kutoa ankara za malipo ya watoa huduma wa meli (Manifest Billing System), pamoja na mfumo wa kutoa huduma za biashara ya Meli,"amesema Bw.Mkeyenge
Pia Mkeyenge amasema katika kuimarisha usimamizi wa usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira dhidi ya shughuli za meli na kupunguza matukio ya ajali za vyombo vya majini TASAC imefanya sensa na kaguzi za vyombo vya usafiri majini ambapo kaguzi 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 zilifanyika na kaguzi 4,490 zilfanyika katika kipindi cha Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023.
"Tumefanya kaguzi za vyombo vya usafiri majini ambapo kaguzi 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 na kaguzi 4,490 katika kipindi cha Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023,"amesema Bw.Mkeyenge
Katika hatua nyingine amesema shirika hilo limefanikiwa Kuboresha ufanisi wa bandari kwa kupunguza uwezo wa shehena inayoruhusiwa kukaa bandarini kwa wakati mmoja (yard density) kutoka asilimia 65 hadi asilimia 50 kwa kuweka Amri ya Tozo ya Bandari Kavu ambapo wamefungua ofisi 11 za Shirika katika maeneo mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi Shirika lina ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Rukwa, Ukerewe pamoja na Geita.
"Kuboresha ufanisi wa bandari kwa kupunguza uwezo wa shehena inayoruhusiwa kukaa bandarini kwa wakati mmoja (yard density) kutoka asilimia 65 hadi asilimia 50 kwa kuweka Amri ya Tozo ya Bandari Kavu ambapo wamefungua ofisi 11 za Shirika katika maeneo mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi Shirika lina ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Kigoma, Rukwa, Ukerewe pamoja na Geita" amesema..
Comments
Post a Comment