UTAFITI WA MBEGU UZINGATIE HALI YA HEWA DKT.JINGU
Pichani : Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu wakati akifungua warsha ya kuelimisha wadau. Kutoka Dodoma Watafiti wa masuala ya kilimo nchini wametakiwa kutumia matokeo ya utafiti wao wanaofanya katika kuboresha mbegu bora za mazao zinazoendana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuwa na tija katika sekta . Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu wakati akifungua warsha ya kuelimisha wadau kuhusu Kazi za Muunganiko wa Taasisi za Kimataifa za Utafiti wa Kilimo (CGIAR) Jijini Dodoma. Dk. Jingu amesema lengo kuu la warsha hiyo ni kuongeza kasi ya utekelezaji wa programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kwa kuboresha uratibu wa miradi ya OneCGIAR kwa kuzingatia utafiti utakaongeza uzalishaji. “Kupitia Mkakati wa Utafiti na Ubunifu wa Mwaka 2030 CGIAR imeanzisha mkakati unaojulikana kama OneCGIAR ambao unalenga kufanya utafiti na maendeleo sasa ili tukuze sekta zetu za kilimo, m