Posts

Showing posts from March, 2023

WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA WIZARA YA AFYA KUONGEZA JITIHADA KWENYE MAGONJWA YA MLIPUKO

Image
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera ,Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene,akizungumza leo leo Machi 22,2023 ,Jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu wa mwaka 2023-2027 wenye kauli mbiu isemayo "Ushirikiano wa Kisekta ni mkakati sahihi wa kuzuia ,kukabiliana na kutokomeza kipindupindu nchini Ifikapo mwaka 2030,". Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera ,Bunge na Uratibu Mhe George Simbachawene, akibonyeza kitufe katika kompyuta kuashiria uzinduzu mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindupindu wa mwaka 2023-2027 wenye kauli mbiu isemayo "Ushirikiano wa Kisekta ni mkakati sahihi wa kuzuia ,kukabiliana na kutokomeza kipindupindu nchini Ifikapo mwaka 2030,". Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel akizungumza leo Machi 22,2023 ,Jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na kipindup

TASAC YATOLEA UFAFANUZI JUU YA UZUSHI WA VIJANA 209 WALIOFUTIWA MKATABA WA MAFUNZO KWA VITENDO KAZINI.

Image
    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bwana Kaimu Mkeyenge akitolea ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Kwenye ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma Machi 10,2023. Na WINNER MARAWITI-DODOMA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bwana Kaimu Mkeyenge ametolea ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan Twitter na Instagram kuhusu malalamiko dhidi ya Shirika hilo yanayosema kuwa Mikataba ya mafunzo kwa vitendo kwa vijana zaidi ya 400 waliokuwa TASAC ilivunjwa bila kufuata utaratibu na ikiwa imebaki muda wa mwaka mmoja kuisha kwa mikataba hiyo. Mkeyenge ametoa ufafanuzi huo Jijini Dodoma Machi 10/2023 wakati akitoa taarifa kwa Umma kupitia waandishi wa habari kuhusu Vijana hao waliokuwa wanafanya shughuli za Mafunzo ya kazi ndani ya shirika hilo. Bwn Mkeyenge amesema kuwa tuhuma walizotoa Vijana hao ni kuwa wanafanya kazi bila bima ya afya na kwamba TASAC ilitoa rushwa kwa Tume ya U

KANISA LA EAGT LAMKABITHI GARI ASKOFU MKUU MWAKIPESILE

Image
  Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Brown Abel Mwakipesile wakati wa Hafla ya kukabidhiwa gari ya Utumishi na kanisa hilo Jijini Dodoma Na.Winner Marawiti,Dodoma. Katika kuazimisha siku ya Wanawake Duniani Kanisa la (EAGT) Dodoma limewataka wakina mama kutambua ratiba ,hasa katika majukumu ya kulea na kutunza watoto pamoja na waume zao kwa sababu mwanamke ndio wenye uchungu zaidi hivyo wanapaswa kuwa na wajibu wenye utaratibu wa kifamilia. Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt. Brown Abel Mwakipesile wakati wa Hafla ya kukabidhiwa gari ya Utumishi na kanisa hilo Jijini Dodoma huku akiwaasa wanadamu kutopumbazika na utandawazi kwa sababu Misingi ya Mungu ipo wazi na inaelekeza namna Mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata mienendo ya Biblia. ''Mimi nasema wanadamu wasizuzuke kwa sababu Misingi ya Mungu ipo wazi Kibiblia Mungu aliweka utaratibu wa mwanadamu anapaswa kuishije kwa sababu kinachokuwa chema kina mipaka yake na mtu kama umeumbwa na utashi wa busara unapaswa kup

JWTZ LATANGAZA NAFASI ZA KUJIUNGA NA JESHI KWA VIJANA WA KITANZANIA

Image
kaimu mkurugenzi wa Habari na uhusiao wa JWTZ, Luteni Kanali GAUDENTIUS ILONDA akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Leo Machi, 9,2023. Na.Winner Marawiti,Dodoma.  Jeshi la wananchi Tanzania limetangaza nafasi za kujiunga na jeshi kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidaato cha nne hadi shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba wa miaka miwili wa mafunzo ya kujitolea katika jeshi la kujenga taifa na kurudishwa majumbani. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari leo march 9 2023 Jijini Dodoma kaimu mkurugenzi wa Habari na uhusiao wa JWTZ, Luteni Kanali GAUDENTIUS ILONDA, amesema nafasi hizo zinawahusu vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu. Aidha,Luteni Kanali ILONDA, ameeleza vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa katika maombi hayo kuwa mwombaji awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na akili timamu,awe na cheti hal

TASAC KUKAGUA MELI 61 ZA KIGENI 2023.

Image
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC),  Bw. Kaimu Mkeyenge  akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma. Na Winner Marawiti. Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), imebainisha kuwa inatekeleza miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini yanazingatiwa. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw.Kaimu Mkeyenge leo Machi 7,2023 Jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TASAC, pamoja na kubainisha Mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkeyenge amesema kuwa TASAC imeunganisha ofisi zake zote zikiwemo zile za Mikoa, Wilaya na mipakani kwenye Mkongo wa Taifa ambao umerahisisha na kuharakisha mawasiliano ya ndani (Intranet), barua pepe, na mawasiliano na wadau wa n

WADAU WA MASUALA YA MAAFA WAJA NA MIKAKATI MADHUBITI YA KUDHIBITI MAAFA

Image
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akihutubia wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 kilichofanyika ukumbi wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma tarehe 7 Machi, 2023. KUTOKA DODOMA. SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa imedhamiria kuwa na mikakati madhubuti katika kukabiliana na maafa nchini. Akizungumza wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Charles Msangi alisema Idara imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa kuhakikisha us

OSHA YAFANIKIWA KUFIKIA ASILIMIA 320 YA UPIMAJI AFYA KWA WAFANYAKAZI.

Image
Mtendaji Mkuu wa OSHA  Khadija Mwenda , wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali na utekelezaji wa majukumu ya Wakala hiyo ,mbele ya waandishi wa habari leo Machi 4,2023,Jijini Dodoma. Na. Winner Marawiti, Dodoma WAKALA wa Usalama na Afya mahala Pa kazi (OSHA),umesema kutokana na kuimarika kwa shughuli za usimamizi wa usalama na afya mahali pa Kazi, umefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 11,953 ongezeko hilo ni sawa asimilia 276 na  idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia Kaguzi 322,241 sawa na asilimia 132. Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa OSHA  Khadija Mwenda , wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali na utekelezaji wa majukumu ya Wakala hiyo ,mbele ya waandishi wa habari leo Machi 4,2023,Jijini Dodoma. "Katika kipindi hiki cha miaka miwili kumekuwa na umarishaji mkubwa sana wa shughuli za usimamizi wa usalama na afya mahali pa Kazi ndio maana usajili wa maeneo y
Image
  Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Samwel Gwamaka akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma akieleza mafanikio ya Baraza hilo katika  kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya  Awamu ya Sita. Na.Winner Marawiti,Dodoma. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC} katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 limepokea na kushughulikia malalamiko takribani 369 ya Uchafuzi na Uharibifu wa Mazingira kutoka kwa wananchi ikiwemo kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya mafuta ,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria. Hayo yameelezwa leo Machi 3,2023Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Samwel Gwamaka wakati akieleza mafanikio ya Baraza hilo katika  kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya  Awamu ya Sita.  Ambapo Dkt.Gwamaka amesema malalamiko hayo yalihusisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, utiririshaji wa maji taka ,uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwandani,kelele za muziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo y

WCF KUBORESHA HUDUMA MUHIMU KWA WADAU NCHINI KWA NJIA YA MTANDAO

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa CHF Dkt.John Mduma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mfuko huo leo Machi 2,2023, Jijini Dodoma  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi {WCF} imeendelea  kuboresha, kuhakikisha  huduma muhimu kwa wadau nchi nzima kwa njia ya mtandao kufikia malengo ya Mfuko huo. Huduma hizo za kimtandao  ni pamoja na Usajili wa wanachama ambapo Mwanachama wa Mfuko huo ni Waajiri, kupata cheti cha Usajili,kuwasilisha michango kila mwezi,Mfuko unnapokea mchango kupitia nambari ya Udhibiti ambayo hupatikana kwa njia ya Mtandao. Hayo yamebaishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt.John Mduma wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mfuko huo leo Machi 2,2023, Jijini Dodoma na kusema hadi kufikia Juni 30 2022 Mfuko umekusanya kiasi cha Shillingi Bilioni 241.48 ikiwa ni kutokana na mapato ya uwekezaji. "Hadi kufikia tarehe 30 June 2022,Mfuko umekusanya jumla ya Shillingi Billioni 241.48 toka kwenye mapato yanayotokana na uwekezaji&quo