Posts

Showing posts from February, 2023

TPHPA YAFANIKIWA KUFANYA UCHAMBUZI WA VIATILIFU 1025

Image
  Na.Winner Marawiti, Mamlaka ya Afya ya Mimea  na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imesema Katika mwaka wa fedha 2022/23, imefanya uchambuzi wa  viuatilifu 10,25 (analysis of pesticide samples) ambapo  sampuli 1005 sawa na asilimia (98.04%) zilikidhi viwango huku sampuli 20(1.96%) ambazo zimeonesha kutokidhi viwango. Hayo yamesemwa  na Dkt .Joseph Ndunguru wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka Hiyo Jijini Dodoma na kusema Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vilisajiiliwa huku Vibali vya shehena za viuatilifu 1324 vyenye ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 ambapo Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu. ''Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji  198 vilisajiiliwa Vibali vya shehena za viuatilifu 1324; ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 Mapato kiasi cha TZS Bilioni 3.06 Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu''Amese

DKT. YONAZI APOKELEWA RASMI NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

Image
                            Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipokea ua kutoka kwa Mwandishi Mwendesha Ofisi  kutoka Ofisi hiyo Bi. Tusekile Mwakangata mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi hiyo,  Februari 28, 2023 Jijini Dodoma.   Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi hiyo, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya mapokezi mara baada ya kuwasili rasmi Ofisini hapo Jijini Dodoma tarehe 28 Februari, 2023.  NA. MWANDISHI WETU- Dodoma Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi  amepokelewa rasmi  katika Ofisi ya Waziri Mkuu  hii leo Februari 28, 2023 Jijini Dodoma na kutoa wito kwa Menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu kwa lengo la kuleta ufanisi. Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Stella Mwaiswaga akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo wakati wa haflaya kumpokea kwa Ka

DKT.NDUMBARO AMEWATAKA VIONGOZI WA TAASISI ZA UTOAJI HAKI KUSHIRIKIANA KATIKA KUONDOA VIKWAZO VINAVYOKWAMISHA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA WATOA TAARIFA

Image
  Na.Mwandishi Wetu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro ,amewataka viongozi wa taasisi za utoaji haki kushirikiana katika kuondoa vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji thabiti wa Sheria ya watoa Taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Dkt.Ndumbaro ameyasema hayo leo Februari 28,2023 Jijini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kanuni za watoa taarifa na Ulinzi wa Mashahidi ,ambapo amesema kuwa  taarifa zinaonesha kuwa utayari wa wananchi kutoa taarifa umeongezeka na walio wengi wako tayari kushiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kufika katika vyombo vya sheria. Amesema kuwa watanzania wakishiriki kwa pamoja katika kufichua maovu yakiwemo yanayosababisha hasara kwa taifa utasaidia kukuza uchumi na kuweka mazingira wezeshi kwa uwekezaji. "Ili tufikie malengo yaliyokusudiwa ya kuhakikisha tunafichua kila aina ya maovu yanayotokea ikiwemo ufisadi,ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka na mengine mengi yaweze kuripo

DOLA 88.4 KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI MANISPAA YA IRINGA

Image
Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji  na usafi wa mazingira mkoa wa Iringa IRUWASA mhandisi David Palanjo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.   Winner Marawiti, Dodoma Katika kuhakikisha wananchi wanaepukana na adha ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini  serikali  imepanga kutekeleza mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika manispaa ya iringa utakao gharimu Dola za kimarekani 88.4. Hayo yameelezwa leo hii Aprili 27,2023 na Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji  na usafi wa mazingira mkoa wa Iringa IRUWASA mhandisi David Palanjo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanukio, mikakati na changamoto za malaka hiyo.  Aidha Mhandisi Palanjo amesema  mradi huo unatarijiwa kuanza mwezi Mei 2023 kwakufanya upembuzi na ujenzi kuanza April 2024 na kukamilika 2027 ambapo kutajengwa mtambo wa kusukuma maji lita milioni 6 kwa siku katika mji wa kilolo.  Sambamba na hilo Mhandisi huyo amebainisha mafanikio yatokanayo na mamlaka hiyo kuwa ni pamoja na kuvuka

MH. SENYAMULE AZINDUA POLISI JAMII CUP DODOMA.

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule katikati mwenye nguo ya blue akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ulinzi na Usalama na baadhi ya wachezaji kwenye uzinduzi wa ligi ya POLISI JAMII CUP DODOMA.  Na. winner Marawiti,Dodoma. Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule, leo 24/2/2023 amezindua  mashindano ya mpira wa miguu Polisi Jamii Cup yaliyoandaliwa  na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mako Makuu katika Uwanja wa Shule ya Msingi central Jijini Dodoma. Katika uzinduzi huo Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Mh.Rosemary Senyamule amewataka wananchi,pamoja viongozi kuanzia ngazi ya kijiji kushirikiana na jeshi la polisi kupitia mradi wa polisi Kata kutoa taarifa za wahalifu kwa Jeshi La Polisi na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Mh.Rorosemary amewasistiza wananchi kuwatumia vizuri polisi Kata walio katika maeneo yao  ili kuweza kutatua migogoro na kutokomeza uhalifu kupitia elimu inayo tolewa na jeshi la polisi kwenye

SERIKALI YAINGIA MAKUBALIANO YA KUANZISHWA KWA KITUO CHA HUDUMA ZA KIBINADAMU NA OPERESHENI ZA DHARURA.

Image
                                              Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mh. Geogre Simbachawene akitia Saini Mkataba wa Makubaliano ya Kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma za Kibinadamu na Operesheni za Dharura cha Jumuiya ya Maendleo Kusini mwa Africa (SADC) jijini Dodoma. Na,Winner Marawiti  Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema itahimarisha na kuendeleza ushirikiano  baina ya nchi Wanachama katika  kukabiliana na maafa, Kuimarisha usalama wa watu na kujenga mazingira rafiki ya shughuli za maendeleo  ili kukuza uchumi. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Mh. Geogre Simbachawene katika Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Makubaliano ya Kuanzishwa Kituo cha Huduma za Kibinadamu na Operesheni za Dharura cha Jumuiya ya Maendleo Kusini mwa Africa (SADC) na kusema Jumuiya hiyo imeendelea kushirikiana katika masuala ya usimamizi wa maafa kupitia Kamati ya Mawaziri wenye Dhamana ya Usimamizi wa Maafa. 

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZINAZOTOKANA NA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO(e_GA).

Image
  Mhandisi Benedict B.Ndomba Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya serikali mtandao(e_GA) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Na. Winner Marawiti. Dodoma. Vijana wakitanzania wameaswa kutumia fursa zinazotokana na mamlaka ya serikali mtandao (e_GA) kwani kupitia mamlaka hiyo wanaweza kuonesha bunifu zao na kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya tehama ili kuendana na kasi ya kidijiti. Hayo yamesemwa na Mhandisi Benedict B.Ndomba Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya serikali mtandao(e_GA) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelezea utekelezaji wa majukumu ya mamlaka ya serikali mtandao (e_GA). "Tunafanya kazi kwa karibu na COSTECH pamoja na vyuo vya elimu ya juu ili kuweza kuwasaidia vijana lakini pia tunawafundisha nini haswa kinachohitajika kwenye fursa zinazotokana na ubunifu wa tehama"Amesema Mhandisi Ndomba. Aidha amesema mamlaka inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi yake mikuu sita(6) ambayo ni uadilifu,ubunifu,kuthamini w

TANESCO KUZALISHA MEGEWATI 5000 ZA UMEME IFIKAPO MWAKA 2025

Image
  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Martin Mwambene akizungumza na wanahabari jijini dodoma. Na Winner Marawiti. kutoka DODOMA Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kupitia  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Martin Mwambene amesema hadi kufikia mwaka 2025 Shirika hilo litakuwa limefikia malengo ya uzalishaji wa Megawati 5000,kutokana na miradi kadhaa ambayo inachangia kuongeza uzalishaji wa umeme katika gridi ya taifa kila mwaka.   Ameyasema hayo  Jijini Dodoma  leo Februari 23,2023,wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali ya shirika hilo na uelekeo wake kwa mwaka wa 2023 ,akiwa na waandishi wa habari.    Aidha amesema kuwa kwa sasa shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 1,820,wakati mitambo iliyopo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,300 pekee.     "TANESCO inafanya miradi kadhaa ambayo inasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka ambapo malengo ni kufikia Megawati 5000 ifikapo 2025,"amesema Mwambene    Mwambene ameong

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA(TCU) KUBORESHA MFUMO WA UBORESHAJI ELIMU YA JUU.

Image
Katibu Mtendaji wa tume Prof. Charles Kihampa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.  Prof.Charles Kihmpa wakati Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa shughuli Mbalimbali za Tume hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita    Na Winner Marawiti.  Kutoka Dodoma. Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU)kupitia wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia imeweka utaratibu wa kuanzishwa na kuimarishwa Mifumo ya uthibiti ubora ndani ya vyuo vikuu ambapo vyuo vyenyewe vimekuwa na utaratibu wa kujikagua, kujitathmini na kufanya Marekebisho mbalimbali kwa kuzingatia Miongozo ya uendeshaji wa vyuo vikuu nchini. Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa shughuli Mbalimbali za Tume hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita leo JIJINI Dodoma, katibu Mtendaji wa tume Prof Charles kihampa amesema mifumo ya ushauri,ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara imefanya vyuo kufanya maboresho makubwa katika miundombinu ya Kufundis

TBA YATEKELEZA MAAGIZO YA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT SAMIA SULUHU HASSAN.

Image
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Ndug. Daud Kondoro akizungumza na waandisi wa habari jijini dodoma. Winner Marawiti, Kutoka DODOMA.  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Ndug. Daud Kondoro amesema kuwa TBA imetekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.,Samia Suluhu Hassan kuhusu bei za nyumba za Magomeni Kota,Jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu huyo ameeleza haya Jijini hapa ,Februari 14,2023, wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo kwa mwaka 2021-2022 na 2022-2023. Kondoro ameeleza kuwa baada ya maagizo ya Rais walikutana na timu ya watalaamu na blogana namna ya kufunga bei ya nyumba hizo. Ambapo amesema kutokana na maelekezo ya Rais wameweza kuondoa shilingi bilioni 18.2 na kwa sasa bei ya nyumba ya chumba kimoja itauzwa kutoka Shilingi Milioni 74.8 hadi Shilingi milioni 48 na ya nyumba mbili kutoka Shilingi milioni 86 hadi Shilingi milini 56.9. “Hii ni kutokana na gharama ya nyumba hizi kwa kuo

WATANZANIA PATENI ELIMU YA MIKOPO

Image
    Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa akizungumza na Wanahabari Jijini Dodoma Februari 13,2023. winner Marawiti Kutoka Dodoma Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa amesema kuwa Watanzania wengi bado hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha itokanayo na mikopo na badala yake wanakopa na kutumia nje ya mipango waliyokusudia. Ameyasema haya Jijini Dodoma, leo Februari 14,2023 wakati akizungumz na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo. Aidha Beng’i ameeleza kuwa pamoja na Serikali kutoa fedha za mikopo kiasi cha shilingi Trilioni 5.6 kwa ajili ya kuwawezesha watanzania milioni 8 bado watanzania wengi wanakabiliwa nakutokua na elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha. “Nataka kuwaeleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana baraza kwa kushirikiana na serikali kwa ujumla wake wametoa kiasi cha sh.tirion 5 .6 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali

SERIKALI YAZIDI KUJIIMARISHA KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAAFA.

Image
  Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao kazi cha kupitia na kujadili Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura kilichofanyika tarehe 16 Februari, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho. Baadhi ya wajumbe wa kikao kazi cha kujadili Rasimu ya Mapango wa Taifa wa Mawasiliano ya Dharura wakiwa katika kazi za vikundi wakiujadili mpango huo.   Kamishna Msaidizi wa Polisi Makao Makuu Dodoma ACP Simon Haule akichangia jambo wakati wa kikao hicho.   Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge (katikati), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa (Kituo cha Operesheni na Mawasilino ya Dharura) Bw. Prudence Constantino (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Mawasiliano ya Simu Wizara ya Habari, Mawasilino na Teknolojia ya Habari Mhandisi Edith Turu